Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Abubakar Kunenge, amepongeza mafanikio makubwa yaliyopatikana katika sekta ya ushirika mkoani humo, akibainisha kuwa ushirikiano madhubuti kati ya serikali, taasisi na vyama vya ushirika umeifanya Pwani kuendelea kuwa kinara kitaifa na kujinyakulia tuzo mbalimbali.
Akizungumza katika Jukwaa la Sita la Ushirika Mkoa wa Pwani lililofanyika Kibaha, Mheshimiwa Kunenge ameeleza kuwa mkoa umepiga hatua kubwa kiuwekezaji, viwanda, afya na uchumi, ikiwa ni pamoja na kuvuka malengo ya ukusanyaji wa mapato kupitia TRA na kushika nafasi ya pili kitaifa kwa mapato ya halmashauri, huku akisisitiza umuhimu wa vyama vya ushirika kupunguza gharama za uendeshaji, kuongeza uwazi, na uwajibikaji ili kuboresha huduma kwa wanachama.




