Naibu Waziri wa Kilimo David Silinde amehitimisha kilele cha Jukwaa la Maendeleo ya Ushirika Mkoa wa Dodoma kilichoenda sambamba na kauli mbiu isemayo "Linda ushirika, chagua uadilifu ".

Akizungumza katika jukwaa hilo leo Juni 6,2026 Mhe. Silinde amewasisitiza wanaushirika kuendelea kuwa waadilifu katika kusimamia na kutekeleza shughuli za ushirika pamoja na kuendelea kutunza maadili yao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa hilo la Ushirika  Ibrahim  Sumbe, amesema pamoja na mafanikio yaliyopatikana bado ushirika unaendelea kukabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo baadhi ya mazao kuuzwa nje ya mfumo wa ushirika. 

Naye Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Dodoma, Joseph Chitinka, amesema kupitia kauli mbiu ya mwaka huu inawahasa wanaushirika kutokujihusisha na vitendo vya udanganyifu.