Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Nurdin Babu amewataka wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro kujiunga kwa wingi kwenye vyama vya Ushirika.
Hayo ameyasema leo Mei 14, 2026 katika ufunguzi wa Jukwaa la tano la Wadau wa maendeleo ya Ushirika litakalofanyika kwa siku mbili mkoani humo.
Aidha, Mhe. Babu amevitaka vyama vya Ushirika kuongeza matumizi ya Tehama ili kuweza kwenda Sambamba na ukuaji wa Teknolojia.
Sambamba na kutoa rai hiyo, Mhe. Babu amepongeza wadau kwa kuweza kutekeleza msingi wa saba wa Ushirika ambapo wameweza kutoa vifaa katika Zahati mbili ambazo ni Zahanati ya Rombo imekabidhiwa kiti na meza ya Daktari, viti viwili vya wagonjwa na benchi moja. Nyingine ni Zahanati ya Siha imekabidhiwa kiti cha nesi, meza moja, kitunza moto na viti viwili vya wagonjwa.
Aidha, ameahidi kuwa pamoja na Wanaushirika katika kusimamia, kuonya na kuongoza. Amewapongeza wadau kuweza kujali jamii kwani wamekuwa wakifanya vitu mbalimbali kama kujenga vituo vya afya, mashule na barabara.




