Watumishi Wanawake wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania wameungana na wanawake wengine wa Jiji la Dodoma katika kuadhimisha Siku ya Wanawake duniani ambayo huadhimishwa Machi 08 kila mwaka. Maadhimisho hayo yaliyobeba kauli mbiu "Wekeza kwa Mwanamke: kuharakisha maendeleo ya Taifa na Ustawi wa jamii" yamefanyika leo tarehe 08 Machi katika Viwanj a vya Shule ya msingi Chinangali Wilayani Chamwino Jijini Dodoma.
Katika kuadhimisha siku ya Wanawake duniani Watumishi hao wameshiriki zoezi upandaji miti katika Shule ya msingi Amani iliyopo Wilaya ya Dodoma Mjini ikiwa ni kutimiza msingi wa saba wa Ushirika " Ushirika kujali jamii" katika kutunza mazingira.
Akifungua maadhimisho hayo Waziri wa Maendeleo ya Jamii,jinsia, wanawake na makundi maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akimwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa(M b)amesema kuwa; serikali inachukuwa jitihada mbalimbali za kuhakikisha kuwa wanawake wanapata fursa na haki sawa katika nyanja zote na kuondoa umaskini kwa wanawake na wasichana.