Wafanyakazi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) Leo Mei 01, 2022 wameshiriki Maadhimisho ya Sikukuu ya MEI MOSI Kitaifa Jijini Dodoma, ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.