Naibu Waziri Mkuu, Dkt. Dotto Biteko, amevipongeza Vyama vya Ushirika nchini kutokana na mageuzi makubwa yanayoendelea kufanyika katika sekta hiyo.
Ametoa pongezi hizo wakati akiongea katika Maadhimisho ya Siku ya Ushirika Duniani Julai 5, 2025 Jijini Dodoma.
Naibu Waziri Mkuu amesema Ushirika umekuwa ukiendelea kuwa na taswira chanya ikilinganishwa na miaka ya awali.
Amebainisha mafanikio hayo ni jitihada nyingi zinazofanyika ikiwepo kuongezeka kwa Hati safi kutoka 339 mwaka 2021/22 hadi 631 mwaka 2023/24 sawa na ongezeko la asilimia 86.13.
Aidha, amepongeza hatua ya kuanzishwa kwa Benki ya Ushirika yenye mtaji wa zaidi ya Billioni 55 ikifanya kazi na matawi manne yanafanya kazi.
Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe, amesema ni muhimu Sekta ya Kilimo kuwa na Sera ya Fedha ya Kilimo itakayosaidia Wakulima kupata huduma za kifedha kupitia thamani ya mazao yao ili kuwapunguzia gharama za upatikanaji wa mitaji.
Maadhimisho hayo yamefanyika kwa kauli mbiu "Ushirika Hujenga Kesho iliyo Bora"