Naibu Katibu Mkuu Elijah Mwandumbya amesema Serikali itaendelea kuimarisha na kusimamia Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) ili viweze kuchochea kasi katika shughuli za kiuchumi za Wananchi.

Amesema hayo wakati wa Uzinduzi wa Taarifa ya Utendaji wa Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS), kwa mwaka 2024 yaliyofanyika Septemba 29, 2025 Jijini Arusha.

Akiwasilisha Taarifa hiyo Mrajis wa Vyama vya Ushirika Dkt. Benson Ndiege amesema Taarifa hiyo inaonesha kukua kwa Ushirika wa Akiba na Mikopo nchini.

Ukuaji huo ulibainishwa na vigezo mbalimbali vilivyotumika ikiwemo Mali za SACCOS kuongezeka kutoka Shillingi Trillioni 1.32 mwaka 2023 hadi Trillioni 1.46 mwaka 2024.

Amesema Utoaji wa Mikopo umeongezeka kutoka Shillingi Trillioni 1.1 mwaka 2023 hadi kufikia Trillioni 1.20 mwaka 2024.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na wawakilishi wa Taasisi mbalimbali ikiwemo Wizara ya Kilimo,  Benki Kuu ya Tanzania, SCCULT, MoCU, TFC, COASCO, DSIK pamoja na SACCOS husika.