Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Brigedia Jenerali Marco Gaguti, amepokea Shilingi Milioni 100 kutoka Vyama Vikuu vya Ushirika vya MAMCU na TANECU kwa ajili ya kuboresha Elimu mkoani Mtwara.

Akipokea fedha hizo zilizotolewa na Vyama vya Ushirika, Brigedia Jenerali Gaguti amesema fedha hizo zitatumika kuhamasisha ufundishaji na ujifunzaji kwa walimu na wanafunzi mkoani Mtwara.

"Fedha hizi zitumike kuchangia katika kuboresha Elimu na zisitumike kulipa posho kwa maofisa waliopo ofisini, ziwafikie walengwa; walimu na wanafunzi katika ngazi zote," amesema Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.