Naibu Waziri wa Kilimo, Mheshimiwa Husein Bashe amefungua viwanda vya kuchakata Pamba (ginnery) vya Chama Kikuu cha Ushirika katika wilaya ya Chato (CCU) cha mkoani Geita na Chama Kikuu cha Ushirika katika wilaya ya Kahama (KACU), mkoani Shinyanga. Uzinduzi huo umefanyika tarehe 8 na 9 Oktoba, 2020. Akiongea kwenye hafla hiyo Mhe. Bashe amesema Serikali ya Awamu ya Tano imeazimia kufufua viwanda vya ushirika vilivyosimama kufanya kazi na ameipongeza Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) kwa kuwa mbele kuhakikisha viwanda hivyo vinarudi kufanya kazi kwa kutoa Mikopo kwa chama cha ushirika CCU pamoja na KACU.