Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu (OWM-KVAU) inatekeleza Programu ya Work Readiness Employability Skills Enhancement (WOREEP) inayolenga kukuza ujuzi wa wahitimu katika Sekta ya Ushirika.

 

Programu hii ni sehemu ya utekelezaji wa Programu ya Kitaifa ya kukuza ujuzi ambayo ndani yake ina kipengele cha mafunzo ya vitendo mahali pa kazi kwa wahitimu (Internship) inayotekelezwa na Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu.

 

Tunapenda kuwajulisha wahitimu wa kada mbalimbali zinazohitajika katika uendelezaji wa Sekta ya Ushirika, watume maombi kwa kujaza fomu maalum zinazopatikana katika tovuti hii: www.taesa.go.tz na kuziwasilisha kwa kuzingatia utaratibu ulioanishwa kwenye tovuti tajwa hapo juu.

 

Mwisho wa kutuma Maombi haya ni tarehe 20 Novemba, 2020.

 

Kwa maelezo zaidi kuhusu zoezi la Kukuza Ujuzi kwa Wahitimu katika Sekta ya Ushirika, tafadhali piga simu zifuatazo: 0754580507 au 0713563014 au tumia baruapepe; doroth.kalikamo@ushirika.go.tz,

 

Imetolewa na:

Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania Bara

TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA

09 Novemba, 2020