Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirikia Tanzania, Dkt. Benson Ndiege,  ametoa wito kwa Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) ambavyo havijajiunga na Chama Kikuu cha Ushirika wa Akiba na Mikopo Tanzania Bara (SCCULT 1992 -  Ltd) wajiunge ili waweze kupata huduma, kuwa na chombo cha kuwasemea na kutatua changamoto zinazowakabili, Utafiti pamoja na kupata fursa za kibiashara ndani na nje ya Nchi.

Pia ametoa pongezi kwa SCCULT (1992) Ltd kwa kuweza kuongeza idadi ya Vyama wanachama wao kutoka 102 mpaka 152 kwa kipindi cha mwaka mmoja na kusisitiza ongezeko zaidi la mabanda

mwakani kwenye Maadhimisho yatakayofanyika mkoani Mwanza. Amesema hayo leo tarehe 19/10/2022 alipokuwa anatembelea mabanda katika maadhimisho ya kitaifa ya 74 ya Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo yanayofanyika Jijini Mwanza.

"Mnafanya kazi nzuri SCCULT (1992) Ltd na nategemea wanachama wote wa SACCOS waliochini yenu wawe na Hati Safi,  wawe wa mfano na hicho ndiyo kivutio cha wananchi walio wengi nje ya mfumo wa Ushirika kujiunga katika Vyama vyenu," amesema Dkt. Ndiege

Pia ametoa wito kwa Vyama vya Ushirika, Wanaushirika wa Vyama nchini na hata kwa wale wasio Wanaushirika kununua Hisa katika Benki ya Ushirika Kilimanjaro