Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt. Benson Ndiege amevitaka Vyama vya Ushirika  kushirikiana na Wawekezaji kwa maslahi ya Wanaushirika kwa kufuata Miongozo ya Uwekezaji.

Dkt. Ndiege ametoa kauli hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi katika Mashamba ya Vyama vya Ushirika yanayoendeshwa na Wawekezaji mbalimbali Machi 13, 2024 Mkoani Kilimanjaro. Akiongea na Wajumbe wa Bodi wa Mradi wa Pamoja wa Mashamba ya Ushirika wa vyama vya Uru kati, Kibosho Mweka Sungu, Uru Shimbwe, Uru East pamoja na Mwekezaji Kilimanjaro Plantation Ltd (KPL) amesema Vyama vinapoweka wawekezaji vizingatie Miongozo ya Uwekezaji wa Mashamba ya Ushirika ili kuleta maslahi kwa wanaushirika na kuepusha migogoro.  

“Hakikisheni mnapotafuta wawekezaji wa mashamba wekeni utaratibu wenye uwazi kwa kutangaza ili kuongeza wigo wa kupata mwekezaji bora, zingatieni bei zinazoendana na wakati na mipaka ya Mashamba ijulikane vizuri kuepusha uvamizi,” amesisitiza Akiongea kwa niaba ya Mwekezaji (KPL) Olga Shuma amesema Mashamba wanayotumia yanazalisha Kahawa tani 600 kila mwaka inayokobolewa katika Kiwanda kilichopo Kilimanjaro Plantation.

 Ameongeza kuwa kutokana na mauzo Mwekezaji anashirikiana na Vyama kwa kutoa Fedha za Msaada kwa Jamii, wanazalisha miche ya Kahawa, wanaendesha Mfuko wa Elimu pamoja na kutoa ajira mbalimbali kiwandani.

Mrajis ametembelea mashamba mengine ya Mradi wa Pamoja wa Ushirika wa Uru North Joint Enterprise, Vaso Agriventure, Wilaya ya Siha Shamba la Lerongo, Shamba la ufugaji Mulomo, Mradi wa pamoja wa Ushirika Wamakikye Shamba la Leon