Wajumbe wa Bodi za Vyama vya Ushirika wametakiwa kusimamia ipasavyo Vyama Vyao ili mali na Wanaushirika ziweze kutumika kuwaletea maendeleo na kuvifanya VYama hivyo kuwa endelevu na kuaminika kwa wadau wake.
Wito huo umetolewa na Naibu Mrajis wa Vyama vya Ushirika (Udhibiti),Collins Nyakunga,leo January 17,2023 JIjini Dodoma katika kikao kazi cha pamoja Kati ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC),Shirikisho la Vyama vya Ushirika (TFC,Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya (COASCO,Bank ya Ushirika Kilimanjaro (KCBL) na Vyama Vikuu vya Ushirika nchini.
Bw.Nyakunga amewataka viongozi wa Vyama vya Ushirika nchini kuhakikisha kuwa Vyama Vyao pamoja na Vyama vilivyoko chini yao vinaondokana na halo mbali ya Ukaguzi na kuhakikisha vitabu vya mahesabu vinaandaliwa ipasavyo na kugaguliwa na Wakaguzi wa Nje.
"Tunatarajia mkitoka hapa mkirudi kwenye Vyama vya Ushirika mpate nafasi mapema kujadiliana na kutekeleza tutakachokubaliana hapa ili kuondokana na changamoto zinazopelekea kupata hati chafu kabla hatua zaidi kuchukuliwa," amesema Nyakunga.
Aidha, Bw Nyakunga amesema kuwa ili kuondokana na changamoto zinazopelekea kupata Hati Chafu inabidi viongozi wa Vyama Vikuu vya Ushirika kutambua majukumu yao, kutambua kazi zao na kufanya kazi kwa kujali miongozo ya Vyama vya Ushirika.
Kikao Kazi kilichofanyika leo kimejadili kuhusu Taarifa ya jumla ya hali ya ukaguzi wa COASCO na mpango wa utatuzi wa dosari zilizobainika katika ukaguzi huo.
Aidha, kikao vilevile kimejadili kuhusu kuimarisha mtaji wa Benki ya Ushirika Kilimanjaro ili kuiwezesha kuwa Benki ya Taifa ya Ushirika, ambapo Naibu Mrajis amevita Vyama Vikuu vya Ushirika kuweka kipaumbele katika kununua Hisa za Benki hiyo.
"Tuangalie namna gani tutakavyoweza kuvitumia Vyama vya Ushirika hususani Vyama ViKuu vya Ushirika kuhakikisha ndani ya muda mfupi tunapata fedha za kutosha ili kuwa na mtaji toshelevu wa Bil.15 ambazo zitatuwezesha kupata usajili wa Benki ya kitaifa ambayo makao yake makuu yatakuwa JIjini Dodoma," amesema Nyakunga.