Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) kwa kushirikisha na Bodi ya Stakabadhi za Ghala (WRRB), Bodi ya Pamba Tanzania (TCB), na Soko la Bidhaa Tanzania (TMX) wameanzisha Mfumo wa kusajili wakulima ujulikanao kama "Mfumo Hub".

Mfumo huo utatumika kwa kuanza kusajili wakulima wa Pamba kwa njia ya kidigitali ambapo utamsaidia Mkulima katika shughuli zote za kilimo ikiwa ni pamoja na upatikanaji  wa pembejeo za kilimo, mavuno, na wakati wa uuzaji wa mazao yake.

Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe amekutana na Taasisi husika leo Februari 7, 2023 Jijini Dodoma na kuridhia kuanza kutumika kwa Mfumo huo ili kumsaidia Mkulima.