Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene,  leo Juni 23, 2023 amezindua Mikataba ya Huduma kwa Mteja ya Taasisi za Umma, ukiwemo wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC). 

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika Jijini Dodoma, Mheshimiwa Simbachawene amezitaka Taasisi zote za Umma kuwa na Mikakati ya Huduma kwa Mteja iliyo hai na kujenga uelewa kwa wateja kuhusu Mikataba ya Huduma kwa Mteja; na Utekelezaji wa Majukumu yake.

Mkataba wa Huduma kwa Mteja unalenga kuwawezesha Watumishi wa Umma kuongeza uwajibikaji na nidhamu ya kazi; kuwa na utamaduni wa utendaji kazi unaojali matokeo na tija kwa wakati; kutenda kazi kwa usikivu na uadilifu; na kuimarisha mahusiano ya kikazi baina ya Watumishi wa Umma na wateja na wananchi kwa ujumla.