Wanachama  sita wa Chama cha Msingi cha Ushirika, Mwamka AMCOS katika Wilaya ya Hanang, mkoani Manyara wamekabidhiwa matrekta manne (4) na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ikiwa ni mkopo wa awali wa matrekta sita (6) yatakayokopeshwa kwa Wakulima hao.

Mkopo huo wa matrekta una thamani ya jumla ya Shilingi milioni 210 unaolenga kuwakopesha matrekta sita, ambapo matrekta manne yamekabidhiwa kwa Wanaushirika hao.