Naibu Mrajis wa Vyama vya Ushirika - Udhibiti, Collins Nyakunga, amewataka Viongozi wa Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) kufanya Uwekezaji na matumizi bora ya TEHAMA, na kuzingatia matakwa ya Sheria, Kanuni na miongozo inayotolewa na Serikali.

Akiongea kwenye wenye Jukwaa la Viongozi wa SACCOS lililofunguliwa jana tarehe 21 Februari 2023 Mjini Korogwe Mkoani Tanga, amewataka Viongozi hao kufanya ubunifu unaoendana na mahitaji ya soko la fedha pamoja na kuzingatia mabadiliko yaliyopo kwenye Sekta ya Fedha pamoja na mahitaji ya wanachama.

"Simamieni vema rasilimali za vyama vyetu ikiwemo kuhakikisha tunapunguza migogoro na malalamiko ya wanachama," amesema Naibu Mrajis.