Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Mhe. Ester Mahawe amevitaka vyama vya wa Ushirika wa Mazao ya Mbogamboga na matunda kuongeza uzalishaji wa mazao hayo ili kuondokana na umasikini.
Ametoa kauli hiyo leo Juni 5, 2024 akifunga mafunzo ya Wajumbe wa Bodi wa Vyama vya Ushirika wa mazao ya Mbogamboga na matunda, Mkoani Songwe.
Amesema vyama hivyo vya Ushirika vikitumia fursa za Ushirika, Kilimo, Miundombinu ya usafirishaji pamoja na matumizi ya teknolojia yataleta chachu kuondoa umasikini.
Aidha, amewataka viongozi hao kwenda kutumia ujuzi wa mafunzo hayo kutatua changamoto za wanaushirika na kutafuta masoko ya ndani na kimataifa.
Nae Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika Hasamba Jacob Mwashamba amesema viongozi hao wapo tayari kushirikiana na wataalamu kuongeza tija ya uzalishaji na kutafuta fursa za masoko.
Katika mafunzo hayo Vyama vya Ushirika Hasamba na Ipunga wamekabidhiwa na Mkuu wa Wilaya vyeti vya usajili wa vyama hivyo. Vyama vingine vilivyoshiriki mafunzo ni pamoja na Tutulane na Haseketwa.