Tume ya maendeleo ya Ushirika Tanzania imeratibu na kufanya kikao kazi na wadau wa zao Mchikichi tarehe 07.10.2022, kilichofanyika ukumbi wa Chuo cha Kikuu cha Ushirika MoCU tawi la Mkoani Kigoma kwa lengo la kukusanya maoni yatakayowezesha mchakato wa uandaaji wa Mwongozo wa uzalishaji, Masoko na Usimamizi wa zao la Mchikichi.

Kikao hicho kilihusisha Maafisa Ushirika na Wakuu wa Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika kutoka Wilaya za Uvinza, Buhingwe, Kibondo, Kakonko, Kigoma, DC. Kigoma Ujiji na Kasulu, Watafiti kutoka Tari- Kihina, Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi(MoCU), Maafisa Kilimo na wawakilishi wa OIfisi ya MKuu wa Mkoa wa Kigoma.

Kupitia kikao hicho, Naibu Mrajis- Uhamasishaji Bi Consolata Kiluma, aliwaeleza washiriki kuwa mwongozo huo utasaidia kuimaridsha sekta ya ndogo ya Chikichi nchini ikiwa ni pamoja na kutumika kuwasilisha na kuwatambua wanunuzi wa Michikichi ghafi, kusimamia na kuendesha masoko na uchakataji wa chikichi, husaidia kuratibu malipo ya wakulima, kuimarisha mfumo wa wa ununuzi na usambazaji wa pembejeo za kilimo, huweka sawa taratibu za uvunaji pamoja na uchakati wa mafuta ya mawese na bidhaa nyingine zitokanazo na Mchikichi.

Aidha aliendelea kusisitiza kuwa zoezi hili nisehemu ya utekelezaji wa maelekezo pamoja na mikakati ya Serikali ya kuwawezesha upatikanaji wa Masoko ya Uhakika wa mazao yatokanayo na Chikichi

Naye Mrajis Msaidizi- masoko na Uwekezaji, Revocatus Nyagilo, aliwaeleza washiriki wa kikao kuwa zao la chikichi linakabiliwa na changamoto kuanzia hatua ya uzalishaji, uchakataji pamoja na kutokuwa zao la kipaumbele hivyo kukosa usimamizi dhabiti na utaratibu wa pamoja.

“Ujio wa Mkakati huu wa uandaaji wa Mwongozo utasaidia katika uwekaji mifumo bora itakayowanufaisha wakulima kupitia upatikanaji wa bei nzuri,ongezeko la uzalishaji na upatikanaji wa ajira kuendeleza sekta ya viwanda, upatikanaji wa miche bora pamoja na matumizi yake kwa usambazaji wa matumizi yake na wakulima.

Washiriki waliipongeza Tume kwa jitihada za kuimarisha mfumo wa zao la mchikichi kupitia AMCOS zilizopo na zitakazianzishwa Kigoma hali itakayopelekea kuongezeka kwa wigo wa uzalishaji na mapato ya serikali na kurahisisha utoaji wa huduma kwa jamii.

MWISHO