Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC) imesaini Randama ya makubaliano (MoU) na Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Januari 27, 2025 Jijini Dodoma katika kuongeza wigo wa ushirikiano na Wadau kwa ili kuimarisha Ushirika nchini.
Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume Dkt. Benson Ndiege akiongea wakati wa utiaji saini wa Randama ya Makubaliano amesema Tume itashirikiana na Chuo kuandaa Mpango wa Maendeleo wa Vyama vya Ushirika ili kutoa Dira ya Maendeleo ya Ushirika.
Aidha amebainisha kuwa ushirikiano huo ni hatua ya utekelezaji wa vipaumbele vya Tume hususani kukuza ushirikiano na Wadau ili kuimarisha Ushirika.
Ameongeza kuwa Tume itashirikiana na Chuo katika kubaini maeneo ya Tafiti kwa kushirikisha Mfuko wa Tafiti ili kutatua Changamoto za Ushirika.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Mipango Prof. Hozen Mayaya amesema Chuo kitashirikiana kutoa Mafunzo, Ushauri elekezi, kufanya Tafiti, wanafunzi kujifunza katika Vyama, pamoja na kupanga Mipango ya muda mrefu na mfupi ya Sekta ya Ushirika.