Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Sophia Mjema ameitaka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) kwenda  kufundisha Mfumo wa Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (MUVU) katika mkoa wa Shinyanga.

Ameyasema hayo leo Oktoba 2022 Kwenye Maonyesho ya Kitaifa ya chakula yanayofanyika kuanzia tarehe 10 Oktoba 2022 hadi 16 Oktoba 2022 Mkoani Simiyu.

Akiwa katika Banda la Ushirika alielezwa na Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Simiyu, Godfrey Mpepo, namna mfumo mpya wa kusimamia vyama vya ushirika ulivyoweza kufanya kazi vyema katika vyama mbalimbali mkoani hapo.

Mhe. Sophia Mjema ameitaka timu inayosimamia Mfumo huo iweze kutoa Mafunzo kwa Wasimamizi wa Vyama mkoani Shinyanga kwa kusaidiana na Ofisi ya Mrajis msaidizi mkoani humo.

Mrajis Msaidizi mkoa wa Simiyu Godfrey Mpepo akimkaribisha Mgeni Rasmi kwenye Banda la Tume ya Maendeleo ya Ushirika katika Siku ya chakula duniani,

Aliweza kumueleza namna walivyofanikiwa katika mfumo huo wa Usimazi wa Vyama vya Ushirika

“Sisi Mkoa wa Simiyu tumekuwa wa kwanza kuanza kutumia mfumo huu umeturahisishia mambo mengi kuhesabu kuvisimamia Vyama hata Kama viko mbali,

Vilevile imerahisisha kuweka uwazi na kuepusha wizi katika Vyama vya Ushirika,” alisema Mrajis Msaidizi

MWISHO