Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania, Dkt. Benson Ndiege ameelekeza Muungano wa Vyama Vya Ushirika wa Akiba na Mikopo Tanzania (SCCULT) kuhakikisha unasimamia Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mkopo (SACCOS) vinaingizwa katika Mfumo wa kidigitali wa Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (MUVU).

Ametoa maelekezo hayo  tarehe 24 Octoba 2023 wakati akitembelea mabanda katika Maadhimisho ya Wiki ya Vyama vya Ushirika vya Akiba na Mkopo Kitaifa Mkoani Mwanza

Amesema Warajisi Wasaidizi wa Mkoa wakishirikiana na SCCULT wataweza kufanya  kazi hiyo kwa ufasaha na uharaka wa kusajili Vyama ili kurahisisha kuwa na takwimu sahihi za Vyama na wanachama wake.

Vile vile ametoa rai kwa Vyama kuendelea kujifunza katika SACCOS nyingine ambazo zilijifunza nje ya nchi ikiwa na lengo la kuweza kusaidia kuboresha SACCOS hizo.