Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde, amewataka Viongozi wa Vyama vya Ushirika na Maafisa Ushirika kufanya kazi kwa werevu, Uadilifu na Uaminifu.

Amesema Viongozi wa Vyama na Maafisa Ushirika wakifanya kazi kwa udilifu itasaidia kujenga imani kwa Wanaushirika na kuongeza idadi ya wanachama katika maeneo yao.

Mheshimiwa Silinde ameeleza hayo Leo tarehe 4 Desemba, 2023 wakati akipokea taarifa ya Ushirika katika Mkoa wa Lindi.

Aidha, amesema ni wajibu wa Vyama na Maafisa Ushirika kutoa elimu kwa wakulima katika maeneo yao ili kuongeza idadi ya wanachama na wawaunganishe wanachama na si kuwatenganisha.

Naye Mrajis na Mtendaji Mkuu Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Dkt. Benson Ndiege, amesema wajibu wa Vyama ni kutengeneza mazingira rahisi ambayo yatarahisisha na kufanya wakulima kujiunga kwa hiari katika Vyama wanavyopeleka mazao yao.

“Wote mnajua kuwa mtu kujiunga na Ushirika ni hiari ila ni wajibu wenu kufanya mambo ambayo yatamvuta Mkulima na kuamua kujiunga na Ushirika kwasababu ndiyo sehemu salama kwa Mkulima,” amesema Dkt. Ndiege. Sent from my iPhone