Mrajis na Mtendaji Mkuu Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania(TCDC), Dkt. Benson Ndiege, amekipongeza Chama Kikuu cha Ushirika cha Kahama( KACU) kwa kuweza kulipa deni la mwaka 2022 na 2023 walilokopa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kwa ajili ya kununua pamba mbegu.

Amesema suala la kukopa na kulipa  ni jambo jema na la kupendeza ambalo linapaswa kufanywa na kila chama kinachokopa ili kujenga imani kwa wakopeshaji na Wanachama.

Mrajis ameeleza hayo leo tarehe 23 Novemba, 2023 alipotembelea Kiwanda cha kuchambua pamba cha KACU kilichopo mjini Kahama.

Aidha, Dkt. Ndiege amewataka viongozi wa KACU kuendelea kufanya mambo yatakayowanufaisha wanachama wao ili wanachama hao wanufaike zaidi na Ushirika wao.