Maafisa Ushirika wametakiwa kutumia maarifa waliyopata kutokana na programu maalum ya mafunzo ya Usimamizi na Ukaguzi wa Vyama vya Ushirika iliyoendeshwa na Tume ya Maendeleo ya Ushirika kwa Maafisa Ushirika kutoka mikoa ya Dar es salaam, Pwani na Morogoro.

Maelekezo hayo yametolewa na Naibu Mrajis, Collins Nyakunga, wakati akifunga Mafunzo ya Maafisa Ushirika Mei 28, 2023 Mkoani Morogoro. Mafunzo ambayo yalizinduliwa Mei 17, 2023 na jumla ya Maafisa 72 wamehudhuria na kupata mafunzo ya Usimamizi wa Vyama vya Ushirika.

Naibu Mrajis amesema lengo la Tume kutoa mafunzo hayo ni kuhakikisha kuwa Maafisa Ushirika wanajengewa uwezo wa kutekeleza majukumu yao vyema ya kusimamia Vyama vya Ushirika ili viweze kujiendesha kwa tija na kupunguza changamoto na ambazo zimekuwepo katika Sekta ya Ushirika.

Sambamba na mafunzo hayo Maafisa Ushirika waliapishwa kutunza Siri mbele ya Hakimu Mkazi Juma Ally Mbonde kwa lengo la kuhakikisha wanasimamia Vyama kwa weledi na kwa kuzingatia maadili ya utunzaji siri ili kuepusha uvujaji wa siri unaoweza kuleta madhara.

Amesema Maafisa Ushirika licha ya Kaguzi wanazofanya mara kwa mara wajikite katika kubaini changamoto na dosari zinazoweza kujitokeza kwenye vyama ikiwemo utatuzi wa migogoro ya vyama pamoja na kufuatilia hoja zinazoibuliwa na Wakaguzi wa nje na kuzifanyia kazi.

Aidha, amewataka Warajis Wasaidizi wa Mikoa pamoja na Maafisa Ushirika kujadiliana masuala ya kiutendaji yanayohusu sekta ya Ushirika kuanzia ngazi za wilaya na mikoa ili pale changamoto zinapobainika ziweze kupata utatuzi wa haraka na pale inapohitajika hatua zaidi taarifa zitolewe na maamuzi yafanyike.

Tume imefanya mafunzo haya ikiwa ni awamu ya tatu, awali mpango huu wa mafunzo ulianza mwaka 2020 katika mikoa ya Kanda ya Kusini na Kanda ya ziwa ambapo maafisa