Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania, Tito Haule, amesema Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Ushirika yatafanyika Julai 5, 2025 Jijini Dodoma.

Akiongea katika Mkutano wa Waandishi wa Habari Jijini Dodoma Juni 26, 2025 amesema Maadhimisho hayo yatatoa fursa ya kuzindua Baraza la Wanawake Wanaushirika Taifa.

Amebainisha kuwa Baraza hilo litatoa fursa zaidi ya Wanawake kushiriki na kuchangia katika shughuli za uzalishaji za Ushirika.

Amesema maadhimisho haya ni fursa ya kukuza utambulisho wa Ushirika, michango ya kujenga uchumi, kukabiliana na changamoto za kijamii na kimazingira.

Akizungumza katika mkutano huo, Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania, Phares Muganda, ametoa wito kwa Vyama vya Ushirika na Wadau kushiriki maadhimisho hayo na kufuatiwa na Maonesho ya Ushirika wakati wa Sikukuu ya Wakulima Nanenane Jijini Dodoma.

Kauli mbiu ya Siku ya Ushirika 2025 ni "Ushirika, Hujenga Ulimwengu Bora kwa wote."