Kuelekea kilele cha siku ya Wanawake Duniani, Watumishi Wanawake wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania wameshiriki Kongamano la Kanda ya Kati( Singida, Dodoma na Iringa)
Kongamano hilo lililokuwa na Mada ya Wanawake na Uongozi katika miaka 30 ya Beijing na kauli mbiu ya “Wanawake na Wasichana 2025 Tuimarishe haki, Usawa na Uwezeshaji limefanyika Leo tarehe 03/03/2025 Jijini Dodoma.