Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe apokea kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo Mifugo na Maji inayoongozwa na Mhe. Christina Ishengoma mbunge waliootembelea katika Shamba la Zabibu lililopo Wilayani Chamwino Mjini Dodoma tarehe 14 machi 2022

Amesema Waziri mkakati uliopo ni kuweka shamba hilo kuwa shamba la mfano  la zao la Zabibu,shamba hilo lenye Hekali 600 linalomilikiwa na Chama cha Ushirika CHABUMA AMCOS lililopo Wilaya ya Chamwino

Ili kupandisha thamani ya Zao hili badala ya kuuza tunda pekee ni kuweka mashine zitakazochakata zabibu na kutengeneza mchuzi ambao utauzwa kwa bei nzuri Zaidi kuliko kuuza tunda pekee “ alisema Mhe. Bashe

Aidha Mwenyekiti  wa Kamati hiyo ya Kudumu ya Bunge Kilimo ,Mifugo na Maji Mhe. Christina Ishengoma ameshauri Tume ya Maendeleo ya Ushirika  kuweka Viongozi makini  wa Vyama hivi vya Ushirika  ili waweze kusimamia Ushirika wao kufika malengo waliyo jiwekea