Baraza la Wafanyakazi la Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) limepitia na kujadili Mpango wa Bajeti ya Tume kww Mwaka 2023/2024.

Bajeti hiyo inategemea kutumika katika ya Matumizi ya kawaida ya  Tume kwa ajili ya Mishahara, Matumizi Mengineyo na Miradi ya Maendeleo.

Mpango huo wa Bajeti wa Tume umepitishwa leo tarehe 24/03/2023 wakati wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika TCDC lililofanyika leo Jijini Dodoma.

Kaimu Mwenyekiti Baraza la Wafanyakazi la Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania, Gabriel Mwita, amewataka wajumbe wa Baraza hilo kurudisha mrejesho wa yaliyojadiliwa katika kikao hiko kwa kuwa wao ndiyo wajumbe wanaowawakilisha watumishi wengine wa TCDC.

Aidha, Bw. Mwita aliwashukuru Wajumbe kwa kufika katika kikao na kuweza kujadili na kupitisha Mpango na Makadirio ya bajeti hiyo ambayo ndiyo muhimili katika Utekelezaji wa Majukumu ya TCDC.