Mwenyekiti wa Bodi ya Makamishna wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Dkt. Abdulmajid Nsekela, amesema sekta ya ushirika ni nguzo muhimu katika kufikia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 inayolenga kujenga uchumi wa Dola za Marekani Trilioni 1.
Dkt. Nsekela ameyasema hayo leo, Agosti 8, 2026 alipotembelea Kijiji cha Ushirika kwenye Viwanja vya Maonyesho ya Wakulima (Nanenane) Jijini Dodoma.
Aidha, alibainisha kuwa hatua inayopigwa na vyama vya ushirika kutoka kujiendesha kwa kiwango cha kawaida hadi kufikia hatua ya kuwa taasisi kamili na imara ni miongoni mwa mafanikio makubwa katika msimu huu wa maonyesho.
"Ushirika unawagusa wananchi wengi, na ndiyo njia sahihi ya kuwafikia watu wote, wawe wa vijijini au wa mijini," alisema Dkt. Nsekela




