Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba amewataka Wakulima na wananchi wanaofika katika maonesho ya Nanenane kuyatumia maarifa wanayoyapata ili kuongeza tija katika Sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi.

Ameyasema hayo Agosti mosi 2026 wakati akifungua Maonesho ya Wakulima Jijini Dodoma ambapo ameeleza maonesho yanatoa fursa kwa wananchi kujifunza teknolojia mpya na mbinu bora za uzalishaji zitakazosaidia kuinua uchumi na kuongeza uzalishaji.

Aidha, amewataka watumishi wa Umma pamoja na wataalam mbalimbali kuongeza uwajibikaji katika Sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi ili wananchi wanufaike zaidi na Uwekezaji unaofanywa na Seikali.

Awali Waziri Mkuu alipata fursa ya kuzindua Mkakati wa Miaka 10 ya ufugaji wa kuku, kutembelea Banda la Maonesho la Vijana,Mdhamini Mkuu wa Maonesho Benki ya TADB, Banda la Ofisi ya Waziri Mkuu, Baadhi ya Taasisi za Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na eneo la malisho ya Samaki.