Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amevikabidhi Vyama vya Ushirika matrekta ya kilimo kwa ajili ya kuendelea kuimarisha sekta hiyo kupitia kuongeza uzalishaji wa mazao nchini.

​Mhe. Rais amekabidhi matrekta hayo leo, Agosti 8, 2026, wakati wa Kilele cha Maonesho ya Siku ya Wakulima (Nane Nane) yaliyofanyika katika Viwanja vya Nane Nane vya John Malecela, Jijini Dodoma. Katika tukio hilo, ameelekeza zana hizo zikatumike ipasavyo ili kuwanufaisha wanaushirika na wakulima wote.

​Matrekta hayo yamepokelewa kwa niaba ya wanaushirika na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC), Tito Haule.

​Maonesho ya mwaka huu yaliyobeba kauli mbinu isemayo "Tambua Soko, Ongeza Tija Kutekeleza DIRA 2050" yamehitimishwa rasmi leo.