Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) imenzindua rasmi Kampeni ya "Linda Ushirika, Chagua Uadilifu".

Uzinduzi huo umefanyika leo  Aprili 24, jijini Dodoma na Waziri wa Kilimo Mhe. Daniel Chongolo kwenye Mkutano wa Wadau wa Maendeleo ya Ushirika.

Mhe. Chongolo ametoa pongezi kwa Ushirika kwa kuonesha njia na kuahidi kuufisha Ushirika unapotaka kwa kuwa lengo ni kusonga mbele zaidi. " Tukisimamia vizuri Ushirika tutapata matokeo mazuri," ameongeza Waziri Chongolo.

Naye Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika , Dkt. Benson Ndiege, amewataka Wanaushirika kuwa na Ushirika imara ambao utaleta Taifa imara sababu Ushirika ni nguzo ya Uchumi wa Tanzania. 

Uzinduzi huo umeudhuriwa na Wadau mbalimbali wa Ushirika ambao ni Taasisi za Kifedha, Shirikisho la vyama vya Ushirika Tanzania bara (TFC), Vyama Vikuu vya Ushirika na Miradi ya Pamoja, Bodi za Mazao, Wizara ya Kilimo, Mambo ya Nje, Viwanda na Biashara, Wadau wa Haki, Kampuni za simu, Wakaguzi wa nje (COASCO) na Wakuu wa mikoa.