Mheshimiwa Peter  Lijualikali, Mkuu wa Wilaya ya Nkasi amevipongeza vyama vya ushirika Mkoani Rukwa kwa kuchangia ukuaji wa Sekta ya Ushirika, ambapo amefurahishwa na utekelezaji wa  kipaumbele cha sita kati ya vipaumbele saba vya Ushirika ambacho ni ushirikiano miongoni mwa vyama vya Ushirika.

Mheshimiwa Lijualikali amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri Mkoani Rukwa kuhamasisha na kutoa elimu ya ushirika kwa wananchi.

Mheshimiwa Lijualikali amesema hayo leo tarehe 5 Juni, 2024 alipomwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa katika Siku ya Ushirika Mkoani Rukwa.

Akitoa taarifa ya Hali ya
ya Ushirika mkoani humo, Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Rukwa,  Marton  Mtindya, amesema Vyama vya ushirika vinavyojihusisha na mazao ya mahindi na mpunga Mkoani Rukwa vimenufaika na mkopo wa shilingi Bilioni 2.1 kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 na 2023/2024.

Maadhimisho ya Siku ya Ushirika mkoani Rukwa yaliyoandaliwa na Jukwaa la Ushirika yamefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Moravian ulioko Sumbawanga mjini.