Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt. Benson Ndiege amesema Tume itaendelea kuimarisha na  kuboresha Sekta ya Ushirika kwa Ushirikiano na Wadau.

Mrajis amesema hayo wakati wa kusaini Hati ya Makubaliano ya utendaji kazi (M.O.U) baina ya Tume na Taasisi ya Agri-Grade Tanzania.

Akiongea katika hafla ya utiaji saini wa Makubaliano hayo amebainisha malengo ya ushirikiano huo ni pamoja na Vyama vya Ushirika kupata mafunzo ya Usimamizi, fursa za masoko ya ndani na nje ya nchi, upatikanaji wa Mitaji na kuviwezesha Vyama kukua kiuchumi.

Kwa upande wake Mwakilishi wa taasisi ya Agri-Grade Japhet Nyangoro amesema watashirikiana na Tume katika kuendesha na kusimamia shughuli za Vyama vya Ushirika.

Taasisi ya Agri- Grade ni muunganiko wa taasisi binafsi za Agritella, IDH, Scope Insight na Oiko Credit.