Chama Kikuu cha Ushirika Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma (TAMCU LTD) Leo Julai 27 kimefanya mnada wake wa Saba katika ofisi za chama hicho ambao  pia  ni mnada wake wa mwisho kwa msimu wa kilimo wa zao hilo

Katika mnada huo mnunuzi mmoja alijitokeza kuomba zabuni ya kununua ufuta wote tani 142 kwa bei ya shilingi 4,789.

Meneja mkuu wa TAMCU LTD Imani Kalembo amewaeleza wakulima wa Wilaya ya Tunduru kuwa mnada huo ni wa mwisho na sasa maandalizi yapo katika kilimo cha zao la mbaazi.

Amesema dhamira ya Chama hicho ni pamoja na kuuza Mbaazi kwa njia ya Stakabadhi ya Mazao Ghalani na wametaka wakulima kuendelea kutumia mfumo huo kwani unawapa uhakika wa soko na bei nzuri ya Mazao yao.

"Sasa ndugu zangu tuwekeze nguvu zetu kwenye kilimo cha mbaazi na korosho ambacho kinatarajia kuanza hivi Karibuni.alisema Kalembo