Chama Kikuu cha Ushirika wa Mkoa wa Pwani, CORECU LTD leo Novemba 01, 2023 kimefanya mnada wake wa Kwanza wa zao la Korosho  katika Wilaya ya Kibiti Mkoani humo
ambapo jumla ya Tani 3,857 zilipelekwa sokoni na kampuni 27 zilijitokeza kuomba zabuni ya kununua Korosho.

Katika mnada huo wa kwanza Meneja Mkuu wa CORECU, Mantawela Hamisi amewasisitiza wakulima kuzingatia ubora wa zao la korosho kwani bei hizo zinatokana na ubora wa Korosho hizo zilikuwa tofauti na za CORECU   na hivyo kuwaomba kuendelea kutunza ubora kwa kiasi kikubwa kwani ubora wa korosho unaendana na bei nzuri.

"Nichukue nafasi hii kuwaomba wakulima wetu kulinda ubora wa Korosho zetu kwani tumeona hapa bei zimekuwa ni za kuridhisha sana kutokana na ubora hivyo tusiendelee kulewa sifa twendeni kukazianike Korosho zetu ipasavyo huu ni mwanzo nzuri sana kwetu," alisema Mantawela.