Kwa niaba ya Tume ya Maendeleo ya ushirika (TCDC), ninayo furaha kuwakaribisha kwenye tovuti yetu mpya ambayo imeboreshwa na kutengenezwa kwa umahiri mkubwa kwa lengo la kuhabarisha umma kuhusu shughuli zinazofanywa na Tume ya Maendeleo ya ushirika(TCDC) hususani katika juhudi za kuboresha utoaji wa huduma katika vyama vya ushirika.
Ni matarajio yangu kuwa tovuti hii itakua ni nyenzo sahihi zitakazoiwezesha jamii kupata habari pamoja na elimu kupitia nyaraka mbalimbali na video ambazo zinapatikana kwa urahisi. Nyaraka hizo ni pamoja na Miongozo, Ripoti, Sera, Sheria, Kanuni pamoja na majarada na vipeperushi. Tovuti hii ina video mbalimbali kwa ajili ya umma na hivyo kuifanya kuwa ni miongoni mwa sehemu muhimu za marejeo katika masuala mbalimbali ya utekelezaji wa shughuri za Tume ya maendeleo ya ushirika.
Mwisho, lakini si kwa umuhimu, natoa wito kwa wadau wote kuendelea kutembelea tovuti hii mara kwa mara na kuwasiliana nasi kwa maoni, ushauri, maboresho au ufafanuzi.
"Ushirika - Pamoja Tujenge Uchumi"
Dkt. Benson O. Ndiege
Mrajis




