TCDC Assistant
Online

Hello. How can we help you today?

Nembo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC)
Nembo ya TCDC
Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
ega-svg-tree

MASWALI NA MAJIBU

Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara

Pata majibu ya maswali yanayoulizwa mara kwa mara.

Mwanachama ana wajibu gani katika chama cha ushirika?
Mwanachama ana wajibu ufuatao: 1. Kulipa ada, hisa na malipo mengine. 2. Kushiriki katika shughuli za kiuchumi za chama. 3. Kuhudhuria mikutano ya chama. 4. Kuteua mrithi inapohitajika. 5. Kulipa madeni kwa chama. 6. Kutekeleza maazimio ya mikutano mikuu. 7. Kulinda mali na maslahi ya chama. 8. Kulinda taswira na sifa za chama. 9. Kukubali mwongozo kuhusu hali zinazoweza kudhuru chama au wanachama. 10. Kutekeleza wajibu mwingine kwa mujibu wa masharti.
Mwanachama ana haki gani katika chama cha ushirika?
Mwanachama ana haki zifuatazo: 1. Kupiga kura na kupigiwa kura. 2. Kuhudhuria na kushiriki mikutano. 3. Kushiriki katika uongozi wa chama. 4. Kuitisha mkutano mkuu maalum kwa mujibu wa kanuni na masharti. 5. Kuchagua mrithi inapohitajika. 6. Kukopa kutoka katika chama. 7. Kumiliki hisa za chama. 8. Kupata taarifa kuhusu masuala ya chama. 9. Kupokea gawio na faida nyingine. 10. Kushiriki kutunga na kurekebisha masharti. 11. Kujitoa katika uanachama. 12. Kuhoji masuala ya chama. 13. Kukata rufaa kwa mujibu wa sheria, kanuni na masharti. 14. Haki nyingine zinazotambuliwa na masharti ya chama.
Ni taarifa zipi zinazopaswa kuwepo katika rejista ya wanachama?
Rejista inapaswa kuwa na: 1. Jina na anwani ya mwanachama. 2. Namba ya usajili ya mwanachama. 3. Idadi na thamani ya hisa zilizolipiwa. 4. Jina na anwani ya mrithi, inapohitajika. 5. Tarehe ya uthibitisho. 6. Tarehe ya usajili wa uanachama. 7. Tamko la kufuata masharti ya chama. 8. Taarifa nyingine zinazohitajika katika masharti ya chama.
Ni kumbukumbu zipi zinazopaswa kutunzwa katika ofisi za chama cha ushirika?
Chama kinapaswa kutunza: 1. Masharti ya chama, marekebisho na nakala za makubaliano. 2. Kumbukumbu za fedha na uhasibu. 3. Mihtasari ya mikutano ya wanachama na Bodi. 4. Notisi za mikutano ya Bodi na mabadiliko yake. 5. Rejista ya wanachama yenye majina, anwani, hisa na mikopo. 6. Rejista ya wajumbe wa Bodi, anwani na tarehe za kuanza au kumaliza uongozi. 7. Rejista ya dhamana iliyoidhinishwa na Mrajis, ikiwa ipo. 8. Kumbukumbu nyingine zinazohitajika kisheria au kwa maelekezo ya Mrajis.
Mrajis wa Vyama vya Ushirika ana mamlaka gani kuhusu taarifa za ukaguzi?
Mrajis ana mamlaka ya kuchukua hatua zinazostahili iwapo chama cha ushirika kitapata hati chafu baada ya ukaguzi.
Mipangilio
Ukubwa wa Maandishi