Hello. How can we help you today?
Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) imeanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 6 ya mwaka 2013 ikiwa ni Idara inayojitegemea chini ya iliyokuwa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi. Baada ya Serikali kuridhia kuibadili kutoka kuwa Idara ya Maendeleo ya Ushirika. Majukumu makuu ya Tume ni kusimamia na kuhamasisha maendeleo ya Ushirika Tanzania Bara. Kisheria Tume ilianza shughuli zake tarehe 1 Januari 2014, ilipotangazwa kwenye Gazeti la Serikali na Waziri mwenye dhamana ya Ushirika, lakini utekelezaji wa majukumu yake kama yalivyoainishwa kwenye muundo wa Tume ulianza mwezi Februari 2015 baada ya kupitishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Maelezo ya Kazi (Job Descriptions) na Mahitaji ya Watumishi (Job List) yalipitishwa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma mwezi Julai 2015.
Tume ya Mandeleo ya Ushirika Tanzania imepewa mamlaka ya kuwa mwangalizi wa uongozi na utendaji kazi wa Vyama vya Ushirika, ikihakikisha kufuatwa kwa Sheria na Kanuni za Ushirika.