TCDC Assistant
Online

Hello. How can we help you today?

Nembo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC)
Nembo ya TCDC
Mamlaka
ega-svg-tree

Wajibu, Majukumu na Kazi


Wajibu
Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania imeanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 6 ya mwaka 2013, na ina mamlaka ya kusimamia na kukuza maendeleo ya sekta ya ushirika.

Majukumu na Kazi
Wajibu wa Tume ni kusimamia na kukuza maendeleo ya sekta ya ushirika kwa kutekeleza kazi zifuatazo:-

Kwa madhumuni ya kusimamia Vyama vya Ushirika, kazi za Tume zitakuwa ni:
(i) Kusajili na kufuta usajili wa vyama vya ushirika;
(ii) Kukagua na kusimamia vyama vya ushirika;
(iii) Kutunza na kuhifadhi daftari la vyama vya ushirika;
(iv) Kuchapisha majina ya vyama vilivyosajiliwa au vilivyofutiwa usajili katika Gazeti la Serikali;
(v) ​​Kutatua migogoro na malalamiko yanayotokana na vyama vya ushirika;
(vi) Kushirikiana na Sekretarieti za Mikoa pamoja na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika utekelezaji wa majukumu ya usimamizi wa maendeleo ya ushirika; na
(vii) Kusimamia utekelezaji wa majukumu mengine ya usimamizi kama itakavyohitajika kwa mujibu wa masharti ya Sheria ya Vyama vya Ushirika.

Kwa madhumuni ya kukuza maendeleo ya sekta ya ushirika, kazi za Tume zitakuwa ni:
(i) Kusimamia, kuratibu na kushirikiana na wizara za kisekta, Mamlaka za Serikali za Mitaa na wadau wengine wanaotekeleza majukumu ya kukuza ushirika;
(ii) Kutoa elimu kwa umma, vijana na makundi mengine kuhusu asili na faida za vyama vya ushirika;
(iii) Kukuza na kuhimiza maendeleo ya vyama vya ushirika imara na endelevu;
(iv) Kuwezesha uanzishwaji wa vyama vya ushirika vinavyowajibika kwa wanachama wake na jamii;
(v) ​​Kutoa elimu na mafunzo kwa wanachama na watumishi wa vyama vya ushirika kuhusu usimamizi wa ushirika;
(vi) Kushauri Waziri kuhusu masuala yote yanayohusiana na maendeleo na usimamizi wa ushirika;
(vii) Kutoa huduma zinazolenga kusaidia katika uanzishwaji, usimamizi, mpangilio na uendeshaji wa vyama;
(viii) Kuratibu mipango ya kiuchumi ya vyama vya ushirika ili iweze kujumuishwa katika mpango wa taifa;
(ix) Kutekeleza au kusimamia utekelezaji wa sera zinazohusu maendeleo ya ushirika. (x) Kuwezesha na kuimarisha mahusiano kati ya wadau, ndani ya nchi na kimataifa;
(xi) Kujenga mazingira mazuri kwa ajili ya ushirikiano na mawasiliano miongoni mwa vyama vya ushirika katika nyanja za uzalishaji, usindikaji, masoko, fedha na uwekezaji;
(xii) Kukusanya na kusambaza, au kusababisha kusambazwa kwa taarifa zinazohusu vyama vya ushirika na maendeleo ya ushirika kwa wadau;
(xiii) Kufanya utafiti unaohitajika kwa ajili ya maendeleo ya vyama vya ushirika;
(xiv) Kushauri vyama vya msingi, vyama vya ngazi ya juu, au aina nyingine za vyama vya ushirika kuhusu uanzishwaji wa shirikisho la vyama vya ushirika; na
(xv) Kuhakikisha kuwa shirikisho hilo lililoanzishwa linatoa, kuandaa na kusimamia huduma madhubuti zilizoratibiwa kutoka ngazi ya kati kwa ajili ya wanachama.

Mipangilio
Ukubwa wa Maandishi