KIKAO CHA 14 CHA KAMISHENI YA TCDC CHAFANYIKA JIJINI DODOMA

KIKAO CHA 14 CHA KAMISHENI YA TCDC CHAFANYIKA JIJINI DODOMA
Kikao cha 14 cha Kamisheni ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) kimefanyika leo Agosti 27, 2026 Jijini Dodoma.
Kikao hicho kimeongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni,Happy Kitingati, na kuhudhuriwa na Makamishna na Menejimenti ya TCDC ikiongozwa na Mrajis na Mtendaji Mkuu wa TCDC, Dkt. Benson Ndiege ambaye ndiye ni Katibu wa Kamisheni.
Aidha, Makamishna na Menejimenti walipata fursa ya kutembelea Benki ya Ushirika Tanzania ( Coop Bank) kwa lengo la kufahamu Mafanikio makubwa yaliyopatikana tangu kuanzishwa kwake na namna wanavyohudumia Vyama vya Ushirika.



