TCDC YAGONGA HODI NJOMBE.

TCDC YAGONGA HODI NJOMBE.
-Yaweka Kambi Kutatua Kero za Ushirika ‘Papo kwa Papo’
Timu ya wataalamu kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), ikiongozwa na Naibu Mrajis - Udhibiti, Collins Nyakunga, leo tarehe 28 Septemba 2026 imewasili Mkoani Njombe kwa ajili ya kuweka kambi maalumu ya kutoa elimu na kutatua changamoto za sekta ya ushirika kupitia kampeni ya “Linda Ushirika, Chagua Uadilifu”.
Kambi hiyo, inayojulikana kama Kliniki ya Ushirika, inalenga kusikiliza kero za wanaushirika na wananchi, kutatua migogoro mbalimbali inayokabili vyama vya ushirika, pamoja na kutoa ufafanuzi na msaada wa kisheria mahsusi kwa sekta hiyo.
Katika kuanza kwa ziara hiyo mkoani humo, timu hiyo imetembelea na kufanya mazungumzo na viongozi wa mamlaka mbalimbali za Serikali kwa lengo la kuimarisha ushirikiano. Miongoni mwa ofisi zilizotembelewa ni pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, pamoja na Ofisi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Njom



