KATIKA KUIMARISHA UWAZI, COASCO YAWASILISHA TAARIFA YA UHAKIKI WA MADENI YA KNCU NA VYAMA VYA MSINGI

KATIKA KUIMARISHA UWAZI, COASCO YAWASILISHA TAARIFA YA UHAKIKI WA MADENI YA KNCU NA VYAMA VYA MSINGI
Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) limewasilisha taarifa ya uhakiki na malinganisho ya madeni kati ya KNCU (1984) Limited na Vyama vya Ushirika vya Msingi wanachama, hatua inayolenga kuimarisha uwazi na uelewa wa pamoja.
Taarifa hiyo imesomwa leo, Oktoba 1, 2026, na Mkaguzi wa Mkoa wa Kilimanjaro, CPA Oscar Mwambungu, katika Ukumbi wa Manispaa ya Moshi, inayohusu kipindi cha miaka 14, kuanzia Mwaka wa Fedha 2011/2012 hadi 2024/2025.
Mkutano huo umeongozwa na Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Dkt. Benson Ndiege, na kuhudhuriwa na Mkurugenzi Mkuu wa COASCO, CPA Alphonce Muro, Mbunge wa Moshi Vijijini, Mhe. Moris Makoi, Mbunge wa Vunjo, Mhe. Enock Koola, pamoja na viongozi na wawakilishi wa KNCU na AMCOS.
Akizungumza katika mkutano huo, Dkt. Ndiege ameipongeza COASCO kwa kazi hiyo na kusema taarifa hiyo itafanyiwa kazi ili kuimarisha zaidi sekta



