TCDC Assistant
Online

Hello. How can we help you today?

Nembo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC)
Nembo ya TCDC
Tunafanya Nini
ega-svg-tree

Mamlaka, Wajibu na Kazi

Tume ya Maendeleo ya Ushirika imeanzishwa chini ya Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 6 ya mwaka 2013. Tume ina mamlaka ya kusimamia, kudhibiti na kuendeleza sekta ya ushirika nchini Tanzania.

Mamlaka, Wajibu na Kazi

Katika udhibiti wa vyama vya ushirika, Tume husajili na kufuta usajili wa vyama vya ushirika, hukagua na kusimamia vyama, hutunza rejesta ya vyama vya ushirika, huchapisha kwenye Gazeti la Serikali majina ya vyama vilivyosajiliwa au kufutiwa usajili, husikiliza na kuamua migogoro na malalamiko yanayotokana na vyama vya ushirika, hushirikiana na Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika utekelezaji wa majukumu ya udhibiti, na hutekeleza majukumu mengine ya udhibiti kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Ushirika.

Katika kuendeleza sekta ya ushirika, Tume husimamia, kuratibu na kushirikiana na wizara za kisekta, Mamlaka za Serikali za Mitaa na wadau wengine wanaotekeleza majukumu ya uhamasishaji wa ushirika. Tume huelimisha umma kuhusu maana na manufaa ya vyama vya ushirika, huhamasisha maendeleo ya vyama imara na endelevu, hurahisisha uanzishwaji wa vyama vinavyowajibika kwa wanachama na jamii, hutoa elimu na mafunzo kwa wanachama na watumishi wa vyama, humshauri Waziri kuhusu maendeleo na usimamizi wa ushirika, hutoa huduma zinazosaidia uanzishaji na uendeshaji wa vyama, huratibu mipango ya kiuchumi ya vyama vya ushirika, hutekeleza sera za maendeleo ya ushirika, huimarisha mahusiano ya wadau ndani na nje ya nchi, huweka mazingira wezeshi kwa mtandao wa ushirika katika uzalishaji, uchakataji, masoko, fedha na uwekezaji, hutunza na kusambaza taarifa za ushirika, hufanya tafiti, hushauri vyama kuhusu uundaji wa shirikisho, na kusaidia mashirikisho kutoa huduma za pamoja kwa wanachama wake.


Mipangilio
Ukubwa wa Maandishi