TUWAJIBIKE KULETA UADILIFU KWENYE VYAMA VYA USHIRIKA

TUWAJIBIKE KULETA UADILIFU KWENYE VYAMA VYA USHIRIKA
Watendaji na wanaushirika wa Vyama vya Ushirika wameaswa kuwa waadilifu, wawajibikaji na kuzingatia misingi ya utawala bora katika utekelezaji wa majukumu yao, ili kuhakikisha Vyama hivyo vinaendeshwa kwa uwazi, uaminifu na kwa kuzingatia maslahi ya wanaushirika.
Wito huo umetolewa leo, Septemba 30, 2026, na Naibu Mrajis Sehemu ya Uhamasishaji, Consolata Kiluma, wakati akifungua Kliniki ya Ushirika kupitia Kampeni ya “Linda Ushirika, Chagua Uadilifu”, inayofanyika katika viwanja vya Stendi ya Zamani, Babati mkoani Manyara.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kliniki hiyo, Kiluma amesema viongozi na watendaji wa Vyama vya Ushirika wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia misingi ya uadilifu, kwani ukuaji wa Vyama hivyo unategemea kwa kiasi kikubwa utendaji mzuri wa viongozi na watendaji wake. “Sisi kama viongozi tunatakiwa tuwe mstari wa mbele katika kuhakikisha tunafanya kazi kwa kuzingatia uadilifu.



