Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji imeipongeza Serikali kupitia Tume ya Maendeleo ya Ushirika kwa kuaandaa Mfumo wa Usimamizi wa Vyama vya Ushirika. 

Waheshimiwa wabunge wa Kamati hiyo wamesema matumizi ya Mfumo huo yatasaidia kuboresha huduma zinazotolewa kwa Wanaushirika kupitia Vyama vya Ushirika Nchini.

Tume ya Maendeleo ya Ushirika imewasilisha Mfumo wa Usimamizi wa Vyama vya Ushirika unaoandaliwa kwa Kamati  Mei 10, 2022 Jijini Dodoma ili kupata maoni yao kabla ya kuanza matumizi ya Mfumo huo.

Waziri wa Kilimo, Mheshimiwa Hussein Bashe, amesema kuwa Maoni na Ushauri uliotolewa na Wabunge utafanyiwa kazi kabla ya Mfumo kuanza kazi.